Home Uncategorized SIMBA:TUNATAKA KUFIKA HATUA YA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

SIMBA:TUNATAKA KUFIKA HATUA YA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa 2020/21 malengo yao makubwa ni kufika hatua ya nusu fainali.


Simba itacheza mchezo wa awali na Plateau United ya Nigeria kati ya Novemba 27-29 nhini Nigeria ambapo kikosi cha wachezaji 24 kinatarajia kuanza safari leo kwa kupitia Ethiopia.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mipango ipo sawa na wanaamini kwamba watakwenda kupambana ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea kwa msimu wa 2020/21 ikiwa ni kuhakikisha wanapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

“Mipango ipo sawa na kila mchezaji yupo tayari, tunakwenda kucheza soka safi na linaloeleweka ndani ya uwanja bila kufanya makosa kama msimu uliopita, mashabiki watupe sapoti,” amesema.
SOMA NA HII  SINGIDA UNITED WAPATA PAKUTOKEA