KLABU ya Barcelona imetinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dynamo Kyiv uliochezwa Uwanja wa NSC Olimpiyskiy.
Bila ya uwepo wa nyota wao namba moja Lionel Messi ambaye alipewa mapumziko na Kocha Mkuu Ronaldo Koeman hakukuwa na tatizo, Barcelona ilipambana na kupata ushindi huo mkubwa.
Martin Braithwaite alikuwa ni nyota wa mchezo huo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufunga na kutoa pasi moja kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Barcelona baada ya kujiunga nayo msimu huu wa 2020 akitokea Klabu ya Leganes.
Mabao ya Barcelona yalifungwa na Sergino Dest dakika ya 52, yale ya Braithwaite alipachika dakika ya 57 na 70 kwa penalti na msumari wa mwisho ulipachikwa na Antonio Griezmann dakika ya 90+2.