Uncategorized

AZAM FC WATIA TIMU MARA KWA WANAJESHI WA MPAKANI

admin November 28, 2020 2:47 pm

 


KIKOSI cha Azam FC kimewasili Mara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United ya Mara maarufu kama wanajeshi wa mpakani.


 Mchezo huo utachezwa Jumatatu, Novemba 30 Uwanja wa Karume na utakuwa ni wa Kwanza kwa Kaimu Kocha Mkuu,  Vivier Bahati kukaa Kwenye benchi.


Bahati amepewa mikoba ya Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi Novemba 26 baada ya kupoteza mchezo mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex. 


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa Bahati ataongoza timu hiyo Kwenye mechi mbili ya Kwanza itakuwa hii dhidi ya Biashara United na ya pili itakuwa dhidi ya Gwambina FC.

VPL: YANGA 1-0 JKT TANZANIA MUUAJI WA AL RABITA FURAHA YAKE IPO HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply