Home Uncategorized UBINGWA WA LIGI KUU BARA WAMPA WAKATI MGUMU KAZE

UBINGWA WA LIGI KUU BARA WAMPA WAKATI MGUMU KAZE


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa shauku kubwa la mashabiki pamoja na viongozi wa Yanga ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara jambo linalompasua kichwa kutimiza malengo hayo.

 Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 13 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaze alisema kuwa anatambua shauku ya mashabiki na viongozi ni kutwaa ubingwa jambo hilo litawezekana ikiwa mashabiki watazidi kujitokeza uwanjani.

“Najua kwamba mashabiki wanahitaji kuona tunatwaa ubingwa hiyo pia ni furaha ya viongozi ila kwa sasa bado tunakazi ya kufanya kwanza ndipo matokeo yatatupa picha ya kile ambacho tunakihitaji.


“Ushindani ni mkubwa jambo ambalo linaleta wakati mgumu katika kufikiria namna ya kufanya na kufikia malengo, kazi ni ngumu ila tuna amini tutafikia kile ambacho tunakifikiria.

“Kwa wakati huu ninaweza kusema neno moja tu kwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kusapoti timu mambo mengine yatafuata,” alisema Kaze.

 

SOMA NA HII  FAINALI YA CECAFA LEO,UGANDA V NGORONGORO