Home Uncategorized HALI YA KIBWANA SHOMARI YAANZA KUTENGAMAA

HALI YA KIBWANA SHOMARI YAANZA KUTENGAMAA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa beki wao wa kulia mwenye jukumu la kumwaga mipira kati kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kuumia bega.


Kibwana ambaye ni mrithi wa viatu vya Juma Abdul alipata maumivu hayo Novemba 25 Uwanja wa Azam Complex wakati timu yake ya Yanga ikiubuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.


Nyota huyo mwenye pasi moja ya bao kati ya mabao 14 yaliyofungwa na Yanga ni chaguo la Kwanza la Cedric Kaze ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.


Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa maendeleo ya wachezaji yapo sawa ikiwa ni pamoja na Kibwana.

SOMA NA HII  NAMUNGO FC:WATATUELEWA TARATIBU, MASHABIKI WATUPE SAPOTI