Uncategorized

BREAKING: NTIBANZOKIZA NYOTA MPYA WA YANGA ATUA BONGO LEO

admin December 2, 2020 8:47 pm

 


BREAKING: SAID Ntibanzokiza mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga, amewasili leo Bongo Desemba 2 rasmi kujiunga na Yanga baada ya kusaini dili la miaka miwili.


Nyota huyo amepokelewa na uongozi wa Yanga ikiwa ni pamoja na wadhamini wake Kampuni ya GSM kupitia Injinia Hersi Said pamoja na Ofisa Uhamasishaji,  Antonio Nugaz.



Pia Ofisa Habari, Hassan Bumbuli naye alikuwepo kwenye mapokezi ya nyota huyo raia wa Burundi.

Nyota huyo ambaye ametua kwa ndege ya usiku akitokea Burundi amepokelewa na mashabiki wengi ambao walijitokeza mapema kuanzia saa 1:00 usiku Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage, Nyerere.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua, mshambuliaji huyo amesema kuwa amefurahi kupata mapokezi makubwa na atapambana kufanikisha malengo ya timu.

Nugaz amesema kuwa kwa uwezo ambao nyota huyo anao lile tatizo la kutofunga mabao mengi litakwishwa na watafanya makubwa. 
KISA HUJUMA, YANGA KUHAMISHIA MECHI ZAKE ARUSHA BREAKING: LWANDAMINA ATUA AZAM FC KUCHUKUA MIKOBA YA CIOABA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply