UONGOZI wa yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara jijini Arusha baada ya kudai kubaini hujuma wanayofanyiwa Dar.
Habari za kutoka ndani ya Yanga zinasema wamekuwa wakishinda kwa tabu kunatokana na njama chafu zinazofanywa na wapinzani wao, zinazosababisha wachezaji kuchoka kabla ya dakika 90 kumalizika.
“Tunadhani kuna mtu yupo ndani yetu anatumiwa, tena inawezekana tupo naye kila siku na anajipenyeza hadi kambini Kigamboni.” kilisema chanzo chetu.
Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrik Mwakalebela hakuweza kuzungumzia suala hilo.