Uncategorized

HESABU ZA SIMBA MBELE YA WANAIGERIA ZIMECHORWA NAMNA HII

admin December 2, 2020 3:47 pm


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa unaamini mchezo wao wa Desemba 5 dhidi ya Plateau United utakuwa mgumu ila watapambana kufanya vizuri ili kupata matokeo chanya.


Simba mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa New Jos, Nigeria iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Clatous Chama kwa pasi ya Luis Miquissone inatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa marudio.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wataingia uwanjani kwa kuwaheshimu wapinzani ila watapambana kupata ushindi ili kufikia malengo waliyojiwekea.


“Tutaingia uwanjani tukiwaheshimu wapinzani wetu lakini hesabu kubwa zipo kwenye kupata ushindi hakuna kingine.


“Tunahitaji kufika hatua ya makundi hivyo hatuwezi kufika hatua hiyo ikiwa tutashindwa kutoka hapa tulipo kwa sasa.


“Mashabiki wajitokeze kwa wingi na mpango wetu namba moja ni kuona kwamba wote watakaoingia uwanjani ni mashabiki wa Simba, hasa ukizingatia kwamba ni mashabiki wachache wanapaswa kuingia kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona,” amesema.

NGORONGORO HEROES YAVULIWA UBINGWA WA CECAFA KISA HUJUMA, YANGA KUHAMISHIA MECHI ZAKE ARUSHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply