Uncategorized

BEKI WA AFRIKA KUSINI AKUBALI KUSAINI SIMBA

admin December 4, 2020 8:47 am


 ABDI Banda, nyota wa zamani wa Klabu ya Simba ambaye alisajiliwa na kikosi hicho msimu wa 2014 akitokea Klabu ya Coastal Union ya Tanga, amesema kuwa yupo  tayari kusaini Simba ikiwa atapewa ofa nzuri kwa kuwa ni timu ambayo inafanikisha malengo ya wachezaji wengi.

Banda alisepa Bongo msimu wa 2017 na kujiunga na Klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini aliyodumu huko mpaka msimu wa 2019 na rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 41 na alifunga mabao manne.

Beki huyo mzawa aliisajiliwa na Klabu ya Highlands Parks ya Afrika Kusini ambayo kwa sasa imeuzwa na kumfanya aache majukumu ya kurudi kwenye timu hiyo mikononi mwa wakala wake na kwa sasa yupo zake Bongo.

Banda amesema:”Ikiwa itatokea nikahitaji timu ya kusaini kwa Bongo, kipaumbele changu cha kwanza ni Simba ukizingatia kwamba ni timu ambayo imenitoa na kunifanya nifikie hapa nilipo, ninajua kwamba wengi wanapenda kusaini Simba.

“Ikiwa nitapata ofa nyingi, kipaumbele changu nitaanza na Simba lakini kitu cha msingi ni maslahi, Simba ni daraja ambalo linawapitisha wengi hata wakiondoka huwa wanakumbuka yale ambayo wamepitia,” .

KMC WAJA NA PIRA KODI MBELE YA DODOMA JIJI FC LWANDAMINA AANZA KUZIPIGIA HESABU SIMBA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply