Uncategorized

KIBARUA CHA KOCHA WA MESSI MASHAKANI

admin December 9, 2020 7:47 am

 


CRISTIANO Ronaldo ameweka mashakani kibarua cha Kocha Mkuu wa Barcelona, Ronaldo Koeman kubaki ndani ya timu hiyo baada ya usiku wa kuamkia leo kukubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Juventus. 


Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa timu hizo ambazo zipo kundi G uliochezwa Uwanja wa Camp Nou , Lionel Messi shujaa wa Barcelona alishindwa kufurukuta mbele ya Ronaldo wa Juventus ambaye aliibuka nyota wa mchezo. 


Ronaldo aliibuka shujaa baada ya kufunga mabao mawili yote kwa penalti dakika ya 13 na 52 na moja lilifungwa ba Weston McKennie dakika ya 20 jambo ambalo limeongeza presha kwa Koeman kufutwa kazi. 


Licha ya kichapo hicho timu zote zimetinga hatua ya 16 bora kwa kuwa zina pointi 15 ila kileleni yupo Juventus.


Koeman amekuwa na mwendo mbovu pia ndani ya La Liga tangu awe ndani ya kikosi hicho msimu huu huku Messi akishindwa kuonyesha makali yake ya zamani.

SIMBA KUFUNGIWA MIAKA MITATU KUFANYA USAJILI NA FIFA LA LIGA KUBADILISHA MFUMO WA YANGA, KUJIENDESHA KISASA NA KIBIASHARA MAMBO YAKIJIPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply