Zinedine Zidane kocha mpya Ufaransa
Habari za michezo

RASMI: Zinedine Zidane Atambulishwa Kuwa Kocha Mpya wa Ufaransa

Vardo July 28, 2026 4:55 pm

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Ufaransa (FFF) leo, Jumanne, Julai 28, 2026, limemtambulisha rasmi gwiji wa soka Zinedine Zidane kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu yao ya taifa.

Zidane (54) amesaini mkataba wa miaka minne wa kuifundisha Ufaransa, akichukua nafasi ya mchezaji mwenzake wa zamani wa Juventus na timu ya taifa, Didier Deschamps.

Deschamps aliondoka kikosini hapo baada ya kukamilika kwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa Kombe la Dunia 2026 dhidi ya England, ambapo Ufaransa ilikubali kichapo cha mabao 6-4.

Uteuzi huu unamrejesha Zidane kwenye ukocha kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2021 alipojiuzulu kuinoa Real Madrid.

Mazungumzo Yaanzia Tangu 2025

Rais wa FFF, Phillipe Diallo, ameweka wazi kuwa FFF ilianza kufanya mazungumzo na Zidane tangu Februari 2025.

“Hii ni nyakati ya kipekee sana. Zinedine ni miongoni mwa magwiji wakubwa wa soka la Ufaransa na kwa miaka mingi amekuwa na ndoto ya kuifundisha timu hii ya taifa. Pia napenda kumshukuru Didier Deschamps na benchi lake la ufundi kwa kazi kubwa waliyofanya kwa miaka 14 kuifanya Ufaransa ibaki kileleni,” amesema Diallo.

Kibarua Chake na Mechi ya Kwanza

Katika mkataba wake wa miaka minne, Zidane anatarajiwa kuongoza Ufaransa kwenye mashindano makuu matatu:

  1. UEFA Nations League (mwaka ujao)

  2. Kombe la Euro (2028)

  3. Kombe la Dunia (2030)

Mchezo wa kwanza wa Zidane akiwa Kocha Mkuu wa Ufaransa utakuwa Septemba 25, 2026 dhidi ya Uturuki katika michuano ya UEFA Nations League.

Wema Sepetu Afunguka Siku 40 ya Mwanae na Ugonjwa