Uncategorized

VITA YA WAJEDA WALIOKUTANA NA MNYAMA UGENINI

admin December 12, 2020 4:47 am

 


BAADA ya kikosi cha Polisi Tanzania kupoteza mchezo wake uliopita Desemba 9 Uwanja wa Mkapa kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Simba, leo inakutana na wajeda Ruvu Shooting Uwanja wa Ushirika,Moshi.


Kikosi kilisepa Dar,Desemba 10 ili kuanza maandalizi ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa ni vita za mbinu za makocha wazawa.


Malale Hamsini wa Polisi Tanzania anakutana na Charles Mkwasa wa Ruvu Shooting ambaye mkononi ana tuzo ya kocha bora ndani ya Ligi Kuu Bara ndani ya Novemba. 


Ikumbukwe kwamba Ruvu Shooting iliinyoosha Simba Uwanja wa Uhuru bao 1-0 na kusepa na pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo ambao nyota wa Simba John Bocco aligongesha kwenye mwamba penalti.


Ofisa Habari wa Polisi Tanzania,  Frank Lukwaro amesema kuwa wanaweka kando matokeo yote mabovu wanaanza upya kusaka heshima.


Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema hawataki utani siku zote wanaingia uwanjani wakihitaji pointi tatu muhimu.


Hivyo leo Uwanja wa Ushirika Moshi ni vita ya wajeda walipokutana na Simba ndani ya Uwanja 

MASHINE YA KAZI INAYOTUA YANGA INA BALAA NDANI YA UWANJA MANCHESTER DABI LEO,GUARDIOLA HATUA KWA HATUA NA OLE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply