Uncategorized

EMMANUEL OKWI AKUTWA NA CORONA

admin December 13, 2020 6:47 am

 


EMMANUEL Okwi mshambuliaji wa kikosi cha Al-Ittihad ya Misri amekutwa na Virusi vya Corona hivyo atakosa mechi kadhaa ndani ya Ligi Kuu ya Misri.


Raia huyo wa Uganda ambaye amecheza pia Ligi Kuu Bara ndani ya Simba na Yanga atakosa mchezo pia dhidi ya Pyramids FC baada ya kukutwa na Corona.


Mabosi wa Al-Ittihad wamethibitisha kwamba Okwi ana Corona na hayupo nchini Misri kwa sasa bado yupo Uganda.

“Safari ya Kurejea kwa mshambuliaji wetu ambaye anacheza timu ya Taifa ya Uganda imesimamishwa baadaye kukutwa na Corona.


“Matokeo hayo ameyapata akiwa nchini Uganda kwani bado hajarejea nchini Msiri nasi tunamuombea apone haraka,” ilieleza taarifa ya klabu. 


Okwi alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda kilichokuwa zikisaka tiketi ya kufuzu Afcon ambapo timu yao ipo kundi B.

MTAMBO WA MABAO NDANI YA AZAM FC KUTUA BONGO LEO VANDENBROECK KUTUMIA JEMBE JINGINE LA KAZI KWA MBEYA CITY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply