JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa kesho ana kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya mabingwa watetezi Liverpool, Uwanja wa Anfield.
Ikiwa ipo nafasi ya Kwanza baada ya kucheza mechi 12 imekusanya jumla ya pointi 25 sawa na wapinzani wao Liverpool ambao wapo nafasi ya pili wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungana.
Tottenham imefunga mabao 24 na kufungwa mabao 10 huku Liverpool ikiwa imefunga mabao 27 na kufungwa mabao 18 ndani ya Ligi Kuu England.
Mshindi wa mchezo wa kesho atakuwa na nafasi ya kuwa kinara huku sare ya aina yoyote kuwa faida kwa Tottenham hivyo Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ana kibarua mbele ya Mourinho.