JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham kesho ana kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England.
Ikiwa ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 12 imekusanya jumla ya pointi 25 sawa na wapinzani wao Liverpool ambao wapo nafasi ya pili wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungana.
Tottenham imefunga mabao 24 na kufungwa mabao 10 huku Liverpool ikiwa imefunga mabao 27 na kufungwa mabao 18 hivyo kesho ni vita ya nafasi ya kwanza ndani ya Ligi Kuu England.
Mshindi wa mchezo wa kesho, Desemba 16 atakuwa na nafasi ya kuwa kinara huku sare ya aina yoyote kuwa faida kwa Tottenham hivyo Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ana kibarua mbele ya Mourinho.
Liverpool ina lundo la wachezaji ambao wataukosa mchezo huo kutokana na kutibu majeraha yao ikiwa ni pamoja na beki wao kisiki Virgil van Dijk, Joe Gomez, Diogo Jota, Thiago Alcatara na Naby Keita.