Home Uncategorized SAIDO NTIBANZOKIZA AANZA NA SINGIDA UNITED,YANGA YASHINDA 3-0

SAIDO NTIBANZOKIZA AANZA NA SINGIDA UNITED,YANGA YASHINDA 3-0

 


INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga kwenye dirsha dogo ambalo limefunguliwa leo Desemba 15, Saido Ntibanzokiza ameanza mchezo wake wa kwanza kwa kufunga mabao mawili ndani ya Uwanja wa Liti.


Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United, Uwanja wa Liti na kushinda mabao 3-0.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Saido dakika ya 22 na dakika ya 66 kwa mkwaju wa penalti na lile la tatu lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 81.

Baada ya mchezo wa leo ambao umeshuhudiwa na mashabiki wengi,nyota huyo amesema kuwa bado anaamini kwamba kuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo ndani ya uwanja.

“Kazi inaanza na kuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo hasa ukizingatia kwamba kila mchezaji anaonyesha ushirikiano ndani ya uwanja.

“Tumeanza vizuri hatuna mashaka katika hili na unapoizungumzia Yanga ni timu kubwa hivyo nasi tunaamini kwamba tutafanya makubwa,” amesema.
SOMA NA HII  MSUVA NA SAMATTA WATUMA UJUMBE MZITO KWA WATANZANIA