Home Uncategorized BERNARD MORRISON AACHWA BONGO SIMBA IKIKWEA PIPA

BERNARD MORRISON AACHWA BONGO SIMBA IKIKWEA PIPA


 KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison ameachwa kwenye msafara wa wachezaji uliokwea pipa leo Desemba 18 kuwafuata wapinzani wao FC Platinum ya Zimbabwe.

Nyota huyo ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe akitokea Klabu ya Yanga kwa dili la miaka miwili amekuwa hana nafasi ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.

Mbali na Morrison nyota mwingine ambaye ameachwa ni Charles Ilanfya ambaye sio chaguo la Sven licha ya uongozi kuweka wazi kwamba usajili wa mchezaji huyo kutoka Klabu ya KMC ilikuwa ni pendekezo la kocha huyo.


Simba imewafuata FC Platinum ikiwa na orodha ya wachezaji 24 ambapo wanatarajiwa kucheza FC Platinum Desemba 23, mchezo wa kwanza kisha ule wa marudiano itakuwa ni kati ya Januari 5-6, Uwanja wa Mkapa.


Nafasi ya Morrison imechukuliwa na kiungo mpya Taddeo Lwanga ambaye  ni ingizo jipya akiwa amesaini dili la miaka miwili.

SOMA NA HII  BAKARI MWAMNYETO ATAJA TIMU ATAKAYOKWENDA, UONGOZI WAFUNGUKIA ISHU YA SIMBA NA YANGA