Uncategorized

SABABU YA BERNARD MORRISON KUACHWA BONGO IPO HIVI

admin December 19, 2020 9:47 am

 


NYOTA wa Klabu ya Simba, Bernard Morrison amesema kuwa kwa sasa bado hajajua nini kinachomsumbua kwa kuwa hajapewa majibu baada ya kulazwa kwenye hospitali iliyopo Dar akipatiwa huduma.


Nyota huyo hayupo kwenye kikosi cha wachezaji 24 waliokwea pipa jana na kuibukia Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.


Simba ilitua salama nchini Zimbabwe na imeanza maandalizi mapema kwa ajili ya mchezo huo wa kwanza unaotarajiwa kuchezwa Desemba 23.

Kwenye Ligi Kuu Bara, Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 na kufunga mabao 33 yeye amefunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Morrison amesema:”Nipo hospitali kwa sasa nilikuwa ninajskia vibaya nikaamua kupata vipimo ili nipate matibabu, baada ya vipimo nitajua nini kinachonisumbua.

Hivyo chanzo cha nyota huyo kuachwa kwenye msafara huo ni kutokana na kutokuwa sawa kiafya jambo ambalo limemfanya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amuache.


Mbali na Morrison nyota mwingine ambaye yupo Bongo ni mshambuliaji, Charles Ilanfya ambaye hajawa kwenye mpango wa Sven.

Chanzo:Championi

SAIDO NTIBANZOKIZA KUANZA NA DODOMA JIJI SEVEN AULA SONY MUSIC ENTERTAINMENT AFRICA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply