Uncategorized

SAIDO NTIBANZOKIZA KUANZA NA DODOMA JIJI

admin December 19, 2020 9:47 am

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umekamilisha kila kitu kuhusu usajili wa nyota wao Saido Ntobanzokiza, raia wa Burundi.


Kiungo huyo mshambuliaji amejiunga na timu hiyo akiwa ni mchezaji huru alikuwa anacheza timu ya taifa ya Burundi.


Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu mchezaji huyo hivyo kuanza kwake leo kwenye mchezo wa Ligi uu Bara dhidi ya Dodoma Jiji ni kazi ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

“Tumekamilisha kupata  leseni na vibali vya mchezaji wetu Saido Ntibazonkiza hivyo kuanza mechi ya leo ni kazi ya benchi la ufundi.

“Maandalizi yapo vizuri na kila mchezaji anajua kwamba tunahitaji kupata pointi tatu hilo lipo wazi kwani mpaka sasa tunakwenda vizuri.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa ni timu nzuri ila wanakutana na timu ambayo ina wachezaji wazuri na wanahitaji pointi tatu,” .

Baada ya kujiunga na Yanga kwenye dirisha dogo, nyota huyo amecheza mchezo mmoja wa kirafiki wakati Yanga ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Singida United.

Uwanja wa Liti ambao zamani ulikuwa unaitwa Namfua yeye alifunga mabao mawili na bao lingine lilifungwa na Deus Kaseke.


DORTUMUND YAPIGWA TENA,MOUKOKO AWEKA REKODI YAKE SABABU YA BERNARD MORRISON KUACHWA BONGO IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply