Uncategorized

NYOTA ALIYEKUWA ANATAJWA KUIBUKIA YANGA ATAJWA AZAM FC

admin December 22, 2020 3:47 pm

IMEELEZWA kuwa nyota wa Klabu ya FC Lupopo inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Congo yupo kwenye rada za kuibukia ndani ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Mwamba huyo anatajwa kuingia kwenye reda za mabosi wa Azam FC ambao wanahitaji kuipata saini yake kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Awali jina lake lilikuwa linatajwa kuingia anga za Yanga inayonolewa na Cedric Kaze baada ya mabosi wa Jangwani kuipata saini ya Saido Ntibanzokiza wameweka kando dili hilo. 

Nyota huyo atapewa mikoba ya Thiery Akono Akono ambaye ameibukia nchini Malysia akitokea Klabu ya Azam FC ambayo alijiunga nayo msimu huu wa 2020/21.

Ofisa Habari wa Azam FC hivi karibuni aliweka wazi kuwa mpango wa kusajili upo na utawekwa wazi kwa kuwa dirisha la usajili bado halijafungwa.

DODOMA JIJI YAZITAKA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR BIASHARA UNITED WAIBAMIZA MABAO 2-0 TANZANIA PRISONS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply