Uncategorized

BIASHARA UNITED WAIBAMIZA MABAO 2-0 TANZANIA PRISONS

admin December 22, 2020 3:47 pm


FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa vijana wake walifuata maelekezo aliyowapa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo jambo lililowapa matokeo chanya.


Leo Desemba 22, Biashara United imebaki na pointi zote tatu Uwanja wa Karume kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons.


Mabao hayo yote mawili yalifungwa kipindi cha pili baada ya muda wa mapumziko kukamilika kwa timu zote kwenda vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa hazijafungana.


Watupiaji wa mabao walikuwa ni Deo Mafie dk 55 na Kelvin Friday dk ya 90 ambaye alikomelea msumari wa mwisho na timu yake kusepa jumla na pointi tatu mazima.

Baraza amesema:”Niliwaambia wachezaji wangu kwamba wana uwezo wa kupata ushindi kwenye mchezo huo ikiwa watatumia makosa ya wapinzani hivyo wanapaswa wawe makini muda wote.


“Nimefurahi kuona kwamba wameweza kutumia makosa ya wapinzani kupata pointi tatu kwetu ni furaha na tunaamini kwamba ni mwendo mzuri ambao tupo nao kwa sasa,” .  

NYOTA ALIYEKUWA ANATAJWA KUIBUKIA YANGA ATAJWA AZAM FC TANZANIA YAISHIA NAFASI YA PILI FAINALI YA CECAFA U 17

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply