NYOTA wa zamani wa kikosi cha Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Mohamed Hussein, ‘Mmachinga’ amesema kuwa Kocha Mkuu wa Simba leo anatakiwa kuanza kwa kujilinda angalau dakika 10 akiwasoma wapinzani wake kabla ya kufanya mashambulizi yakushtukiza.
Simba chini ya Sven Vandenbroeck ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo itacheza na FC Platinum ya Zimbabwe kabla ya kurudiana nao kati ya Januari 5-6, Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mmachinga amesema kuwa mbinu itakayompa matokeo mapema Sven ni kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza kwa kuwa watakuwa ugenini.
“Watakuwa ugenini na wanacheza na timu ambayo ni imara hivyo itakuwa kazi kwa Simba kushinda mapema zaidi wanatakiwa waanze kujilinda huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza angalau baada ya dakika 10 kupita.
“Mwanzoni kila mtu anakuwa anasoma mbinu za mpinzani wake sasa kwa soka letu la Afrika lilivyo inajulikana kwamba mwenyeji anabaki kuwa mwenyeji tu hivyo lazima Simba wajilinde na kufanya mashambulizi yakushtukiza,” amesema