Home Uncategorized MTAMBO MPYA WA AZAM FC WAANZA KAZI

MTAMBO MPYA WA AZAM FC WAANZA KAZI


  NYOTA mpya ndani ya Klabu ya Azam FC ambaye ni mshambuliaji Mpiana Monzinzi, baada ya kusaini dili la mwaka mmoja jana Desemba 23 alianza kufanya mazoezi na timu hiyo.

 Mozinzi alitua Desemba 22 akitokea nchini Congo kwa ajili ya kuja kufanyiwa vipimo na mara baada ya kila kitu kwenda sawa alisaini dili hilo na kwa sasa ni mali ya Azam FC.

Amekuja kuchukua mikoba ya Akono Akono raia wa Cameroon ambaye alikuwa ni mshambuliaji wa Azam FC yeye amesepa Bongo baada ya kupata dili nchini Malysia.

Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Azam Sports (ASFC) ambapo kitacheza dhidi ya Magereza.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Azam Complex Jumamosi ya Desemba 26 saa 1.00 usiku.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa ujio wa nyota huyo utaongeza nguvu na kasi ya kikosi hicho ambacho kinawania taji la Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MALENGO YA OZIL NI KUMALIZANA NA MABOSI WAKE KWANZA NDANI YA ARSENAL