Uncategorized

SIMBA KUTUA TIMU BONGO LEO

admin December 24, 2020 9:47 pm

 


BAADA ya kupoteza mchezo uliochezwa Desemba 23 wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum,  kikosi cha Simba leo kinatarajiwa kutua ardhi ya Bongo.

Simba ilikamilisha dakika 90 law kufungwa bao 1-0 ambalo lilipachikwa dakika ya 17 na Perfect Chikwende kwa jitihada binafsi baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Wekundu  Msimbazi. 

Mchezo wa marudio utakuwa Januari 6 2021, na Simba inatakiwa kushinda mabao zaidi ya mawili ili kutinga hatua ya makundi.


Kocha Mkuu wa Simba,  Sven Vandenbroeck amesema kuwa watajitahidi kuongeza umakini ili kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.


Jumapili, Desemba 27 ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Majimaji FC mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya tatu.

NAMUNGO YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply