KOCHA wa Klabu ya Coastal Union Juma Mgunda amesema kuwa ataongeza nyota wawili kwenye safu ya ushambuliaji ili kukipa nguvu kikosi chake.
Coastal Union imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ambapo ipo nafasi ya 13 na pointi zake 19.
Safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 10 baada ya kucheza mechi 17 jambo ambalo limemfanya Mgunda kufikiria kuongeza nguvu kwenye upande wa washambuliaji.
Mgunda amesema:”Nina kikosi kizuri chenye wachezaji ambao wanajituma ila ni muhimu niongeze washambuliaji ili kuwapa nguvu zaidi hawa waliopo hivyo ni suala la kusubiri na kuona mambo yatakuaje,” .