Uncategorized

BAADA YA KUPIGWA 5G,MAJIMAJI WATAJA ALIYEWAPONZA

admin December 29, 2020 1:47 am


 KIPA namba moja wa Klabu ya Majimaji, Mputi Jafary amesema kuwa uwezo wa kiungo wa Simba, Said Ndemla ulichangia kwa timu hiyo kupoteza mchezo huo kufungwa mabao 5-0.


Jafary alikaa langoni ndani ya dakika 90 ambapo aliokoa shuti moja la Ndemla dakika ya 15 na kusababisha kona na pia dakika ya 3 alikutana na shuti la Ndemla ambalo liligonga mwamba kabla ya kukutana na guu la Gadiel Michael aliyezamisha mpira wavuni.

Jaffary amesema:”Mabao matano ni mengi na yanaumiza kwa kuwa hatukutaka kufungwa ila kushinda mchezo na kusonga hatua ya mbele.


“Ila nyota aliyesababisha yote  yatokee ni yule kiungo Said Ndemla alikuwa anacheza na mpira namna anavyotaka na kuisumbua timu muda wote aliokuwa ndani ya uwanja.


“Ukiachana na hilo pia sehemu ya viungo wa Simba hapo ndipo ambapo palituharibia utulivu pia viungo wao muda wote walikuwa wanamiliki na kutengeneza hatari,” .


Simba Desemba 27 iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho na kusonga mbele.


Mabao Uwanja wa Mkapa yalifungwa na Gadiel Michael, Chris Mugalu,Ibrahim Ame, Meddie Kagere na Luis Miquissone. 

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE BEKI KITASA WA SIMBA KUIBUKIA AFRIKA KUSINI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply