Uncategorized

RUVU SHOOTING: MWENDO WETU NDANI YA LIGI KUU BARA NI ULEULE

admin December 29, 2020 4:47 pm


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa kikosi chao kitaendelea kutoa soka la darasani ili kuleta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa mwendo wao ndani ya Ligi Kuu Bara hautazima kwa kuwa wana wachezaji wazuri pamoja na mwalimu mwenye uzoefu.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Ruvu Shooting ipo nafasi ya tano ikiwa imekusanya pointi 26 baada ya kucheza mechi 16.

Bwire amesema:”Tupo imara na hatuna mashaka ya kile ambacho tunakifanya ndani ya ligi mpaka pale tutakapofikia malengo yetu.

“Vijana wetu wanacheza kwa kujituma na morali ni kubwa ndani na nje ya uwanja hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti.

“Tutaendelea kutoa mpira wa darasani na kuonyesha juhudi ndani ya uwanja. Mashabiki wasiache kutupa sapoti bila kuchoka,” .

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA KILICHOITWA KWA AJILI YA MICHUANO YA CHAN MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply