Uncategorized

JONAS MKUDE ATAJA CHIMBO LAKE LILIPO

admin January 1, 2021 10:47 am


 JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya Klabu ya Simba ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ametaja pale alipo kwa sasa baada ya kuchimbishwa ndani ya kikosi hicho.

Mkude alisimamishwa na Klabu ya Simba, Desemba 28 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu na anatarajiwa kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ili aweze kujibu tuhuma ambazo zinamkabili.

Kwa msimu wa 2020/21, Mkude amecheza jumla ya mechi 10 kati ya 15 ambazo timu yake ilikuwa imecheza jambo linalomaanisha kwamba ni Sven anakubali uwezo wake.

Mkude amesema kuwa yupo ndani ya ardhi ya Dar kwa sasa huku akigoma kuzungumzia sakata lake na Simba.

“Nipo salama kwa sasa ninaendelea vizuri hapa Dar ila kuhusu masuala hayo mengine unayotaka sitazungumza kwa sasa,” amesema Mkude.


Chanzo:Spoti Xtra

KANE AINGIA ANGA ZA MANCHESTER CITY SportPesa YAMWAGA MAMILIONI KWA NAMUNGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply