Uncategorized

LEO NI VITA YA TANO BORA ENGLAND, BRUNO NOMA

admin January 1, 2021 1:47 pm


LEO Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkjaer ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Aston Villa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.


Hii ni vita ya tano bora kwa kuwa timu zote zimekuwa na mwendo mzuri kwa msimu wa 2020/21.

Ikiwa ilianza kwa kusuasua United ghafla imewaka na kuanza kukimbizana kwenye pointi na Liverpool ambapo ikiwa itashinda leo itafikisha jumla ya pointi 33 ambazo zipo mikononi mwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo.


Ikumbukwe kwamba United iliwahi kukutana na kichapo cha mabao 6-1 kutoka kwa Tottenham huku Liverpool ikipokea kichapo cha mabao 7-2 kutoka kwa Aston Villa.


Ndani ya United Bruno Fernandes akiwa amecheza jumla ya mechi 15 ametupia mabao 10 na pasi 7 za mabao.

Kwa Aston Villa iliyo nafasi ya tano na pointi 26 wao wanaye Ollie Watkins mwenye mabao sita na pasi mbili kwenye mechi 14 ambazo amecheza ndani ya Ligi Kuu England.

SportPesa YAMWAGA MAMILIONI KWA NAMUNGO MZAMBIA WA SIMBA ASAINI KWA WAARABU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply