Uncategorized

KAGERE AFUNGUKIA ISHU YA BABAYE

admin January 5, 2021 5:47 am


 MSHAMBULIAJI wa Simba, raia wa Rwanda, Meddie Kagere, ameibuka na kusema kuwa, yeye si Mtanzania na hamtambui mzee anayesema ni baba yake.

 

Hivi karibuni, mzee Vedasto Katologi, aliweka wazi kuwa yeye ni baba wa nyota huyo kwa kusema ikiwa Kagere atakuwa tayari kuonana naye yupo tayari wakapime DNA.


 Mzee huyo ambaye ni mkazi wa Bukoba anasema kuwa anakubali uwezo wa nyota huyo na anaamini ni babaye kwa sababu aliwahi kumpa mimba mwanamke ambaye amemsahau.


 Kagere amsema: “Eti kuna mtu anasema yeye ni baba yangu? Hapana, sina taarifa hizo na sijawahi kuongea naye, aache uzushi, mimi sina undugu naye.”

 

Kagere aliyejiunga na Simba msimu wa 2017/18 akitokea Gor Mahia ya Kenya, huu ni msimu wake wa tatu ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa kinara wa ufungaji katika ligi hiyo kwa misimu miwili mfululizo.


Chanzo:Championi 

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE MTAMBO WA MABAO YANGA WAPEWA MASHARTI MAGUMU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply