Home Uncategorized YANGA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA MAPINDUZI

YANGA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA MAPINDUZI


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unahitaji kurejea kwenye ardhi ya Tanzania Bara ikiwa na Kombe la Mapinduzi.

Tayari kikosi kimewasili Visiwani Zanzibar, jana Januari 4 na leo kitaanza kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Chipukizi mchezo utakaochezwa majira ya saa 8:15 usiku Uwanja wa Amaan.

Kikosi cha kwanza kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kimetia timu visiwani Zanzibar ikiwa ni pamoja na kipa namba moja Metacha Mnata ambaye ni chaguo namba moja la Mrundi huyo.


Yacouba Songne, Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, Saido Ntibanzokiza na Carlos Carlinhos ni miongoni mwa nyota waliopo kwenye kikosi.

Akizungumza Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini kwamba watafanya vizuri kwenye mechi zao.

“Nguvu yetu na malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu ndani ya Kombe la Mapinduzi, mashabiki wazididi kutupa sapoti,” .

SOMA NA HII  KOCHA MTIBWA SUGAR: TAHADHARI YA CORONA NI LAZIMA IFUATWE NA WATU WOTE