Uncategorized

AZAM FC YAWASILI ZANZIBAR,KESHO KUANZA KAZI

admin January 6, 2021 11:47 am


 KIKOSI cha Azam FC, leo Januari 6 kimewasili salama visiwani Zanzibar ambapo kimekwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.


Tayari michichuano hiyo imeshaanza kurindima na jana Januari 5, mabingwa watetezi Mtibwa Sugar walifungua pazia kwa kumenyana na Chipukizi, Uwanja wa Amaan na kupata ushindi wa bao 1-0.


Azam FC itafungua pazia la michuano hiyo kwa kukipiga dhidi ya Mlandege, kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Amaan saa 2.15 usiku.


Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamini ina kazi ya kusaka ushindi ili kuweza kufikia malengo ya kutwaa taji hilo ambalo walipokwa msimu wa 2020 na Mtibwa Sugar.

MAJEMBE MATATU YA KAZI NDANI YA SIMBA KUWAKOSA FC PLATINUM LEO SIMBA INA KAZI KUBWA YA KUFANYA LEO MBELE YA WAZIMBABWE, REKODI HAZICHEZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply