Uncategorized

MAJEMBE MATATU YA KAZI NDANI YA SIMBA KUWAKOSA FC PLATINUM LEO

admin January 6, 2021 11:47 am


 TADDEO Lwanga, ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba kuna hatihati ya kuukosa mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum kutokana na kusumbuliwa na majeraha.


Nyota huyo raia wa Uganda ambaye ni kiungo mkabaji alipata majeraha hayo kwenye maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Majimaji.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 5-0 na kiungo huyo ambaye ameletwa kumpa changamoto kiungo Jonas Mkude hakuwepo.

Pia Lwanga ambaye alikwea pipa na Simba kuelekea nchini Zimbabwe kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum hakuwa kwenye kikosi kilichopoteza kwa kufungwa bao 1-0 mchezo wa kwanza kwa sababu vibali vyake vilikuwa havijakamilika.


Nyota mwingine mbali na Jonas Mkude ambaye anatumikia adhabu kutoka kwa Simba kutokana na utovu wa nidhamu pia nyota Charlse Ilanfya yeye ameondolewa kwenye mpango wa Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.

MTIBWA SUGAR YAPANIA KUFANYA VIZURI MAPINDUZI AZAM FC YAWASILI ZANZIBAR,KESHO KUANZA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply