KLABU ya Simba inasubiri droo itakayopangwa leo Januari 8, 2021, Cairo, Egypt kujua wapinzania wao baada ya kufuzu hatua ya makundi Januari 6, 2021 Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba imefika hatua hiyo baada ya kushinda mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe licha ya kufungwa bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa Zimbabwe.
Timu zote zimetengwa kwenye makundi (pot) nne kutokana na pointi walizonazo na Simba ipo pot 3 na timu za Petro de Luanda ya Angola na MC Alger ya Algeria.
Katika pot hiyo Simba watasubiri timu moja baada ya kutochezwa kwa mechi ya marudiano ya Al Hilal ya Sudan dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana baada ya Kotoko kugoma kucheza kwa madai mchezaji wao mmoja hajapatiwaa majibu yake ya vipimo vya corona.
Kwa mantiki hiyo Simba atasubiri timu za pot 1, 2 na 4 ambazo zipo hivi;
Pot 1 – Al Ahly (Misri), Wydad Casablanca (Morocco), Esperance (Tunisia), TP Mazembe (Congo).
Pot 2- Zamalek (Misri), Mamelod Sundown (Afrika Kusini), Horoya (Guinea), AS Vita (Congo)
Pot 4- Al Merrikh (Sudan), CR Belouizdad (Algeria), Teungueth (Senegal), Kaizer Chiefs (Afrika Kusini)