Uncategorized

ARGUERO ANUKIA KUIBUKIA PSG

admin January 10, 2021 8:47 am

 


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Paris Saint-Germain,(PSG) Mauricio Pochettino anahitaji saini ya mshambuliaji wa Manchester City,Sergio Aguero. 

Kwa mujibu wa wakala, Bruno Satin ambaye aliwahi kusimamia ishu ya usajili wa Michael Landreau ambaye ni kipa wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufarasa na kwa sasa mchezaji huyo ana umri wa miaka 41.

Satin amesema kuwa Pochettino anahitaji kumfanya Arguero kuwa saini yake ya kwanza ndani ya kikosi hicho cha PSG baada ya kuanza kazi akiwa amesaini dili la mwaka mmoja lenye kipengele cha kuongeza mkataba ikiwa atafanya vizuri baada ya kupokea mikoba ya Thomas Tuchel.

 Arguero mwenye miaka 32 ni mtambo wa mabao ndani ya City inayonolewa na Pep Guardiola kwa sasa anaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu nyingine kwa kuwa mkataba wake ndani ya kikosi hicho umebakiza miezi sita.

DECLAN RICE AGOMEA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED MITAMBO HII YA MABAO YANGA ILILETWA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply