Uncategorized

MITAMBO HII YA MABAO YANGA ILILETWA LEO

admin January 10, 2021 10:47 am


MICHEL Sarpong, mshambuliaji wa Klabu ya Yanga ambaye alijiunga na Klabu hiyo akitokea Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda leo anatimiza umri wa miaka 25 baada ya kuletwa duniani.


Rekodi zinaonyesha kuwa mshambuliaji huyo mwenye mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara aliletwa duniani Januari 10,1996.

Mbali na Sarpong nyota mwingine wa Yanga ambaye naye pia ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani ni mshambuliaji, Yacouba Songne ambaye naye pia ametupia mabao mawili ndani ya ligi.

Mbali na kutupia mabao hayo ametoa pia jumla ya pasi nne ambazo zilileta mabao kwa msimu wa 2020/21.

Rekodi zinaonyesha kwamba Songne raia wa Burkina Faso aliletwa duniani Januari 10, 1992 anatimiza umri wa miaka 29.
ARGUERO ANUKIA KUIBUKIA PSG NI SIMBA V NAMUNGO NUSU FAINALI, YANGA YAMSUBIRI MSHINDI WA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply