KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa wamekuwa kwenye mwendo mbaya ndani ya Ligi Kuu England hivyo wana kazi ya kufanya mbele ya Manchester United.
Liverpool inakutana na Manchester United ambayo gari limewaka baada ya kushinda mechi zake tatu zilizopita ndani ya Ligi Kuu England ambapo ilishinda mbele ya Wolves bao 1-0, ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnely kwa bao la Paul Pogba uliwapeleka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wanakwenda mwendo wa kusuasua baada ya kushinwda kupata ushindi kwenye mechi tatu mfululizo ndani ya Ligi Kuu England ambapo ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na West Brom kisha ikaambulia sare ya bila kufungana na Newcastle United na mchezo wake wa mwisho ilichapwa bao 1-0 dhidi ya Southampoton, Uwanja wa St Mary’s
Wakati Klopp akisema kuwa wanahitaji kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho utakaochezwa Uwanja wa Anfield, Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajer amesema kuwa nao pia wanahitaji pointi tatu ili kuzidi kujikita kileleni.
Klopp amesema:”Tumepoteza mchezo wetu uliopita mbele ya Southampton na kiukweli ilikuwa ni maumivu kwetu wala hatukuhitaji jambo hilo litokee ila kwa kuwa limetokea hatuna namna ya kuzuia.
“Lakini niliweza kuongea na wachezaji na wanajua sehemu ambayo tunataka kuwa hivyo hilo lipo wazi tunajua kwamba tutakuwa na mchezo mgumu tunaangalia kile kijacho mbele yetu kwa uaminifu kabisa na mchezo wetu huu ujao tutafanya vizuri ili kuondoka kwenye hali hii mbaya ambayo tupo kwa sasa,” amesema.
Ole amesema :”Ni nyasi za kijani na mistari ile yenye rangi nyeupe siku zote huwa uwanjani hivyo ni kawaida tu hakuna mashaka, ukichukua muda ambao tumekuwa ndani ya Anfield kwetu ni faida na tunakwenda kufanya kazi,” .