Home Uncategorized MORRISON:MPIRA SIO VITA, NILIKUWA YANGA SASA NIPO SIMBA

MORRISON:MPIRA SIO VITA, NILIKUWA YANGA SASA NIPO SIMBA

 

KIUNGO wa Klabu ya Simba, Bernard Morison amesema kuwa maisha ya mpira sio vita bali ni kazi ndani ya uwanja hivyo kila kitu kwakwe anajifunza.

Nyota huyo aliibuka ndani ya kikosi cha Simba akitokea Yanga ambapo uhamisho wake umekuwa na vurugu nyingi hasa kufuatia mabosi wake wa zamani Yanga kudai kwamba bado ni mali yao.

Ndani ya Simba hajawa akionekana kikosi cha kwanza tofauti na alipokuwa Yanga ambapo mabosi wa Simba wameeleza kuwa ana matatizo ya kiafya ambayo yatamuweka nje kwa muda wa miezi sita.

Habari zinaeleza pia huenda ikawa mwisho kwa nyota huyo mpanda mpira kuwa na jezi za Simba kwa kuwa kuna ingizo jipya ambaye ni Perfect Chikwende ataziba nafasi yake.

Morrison amesema:-“Maisha ya mpira sio vita,watu wanapaswa waelewe kwamba nimeishi Yanga kwa furaha na sasa nipo ndani ya Simba maisha yanaendelea.
“Kikubwa ni kwamba kila sehemu kuna furaha na kila timu ni bora. Unaweza kusema kwamba ninaweza kusema vibaya kuhusu Yanga hapana hiyo sio sawa,tatizo wengi wanafikiria mabaya kule ambako ulikuwa,” .
SOMA NA HII  UNAAMBIWA SIMBA WALICHEZA PIRA GIMBI DHIDI YA WYDAD MCHAMBUZI AFUNGUKA HAYA