Yanga SC

MKWASA AFICHUA KINACHOMBEBA KAZE

admin January 20, 2021 1:47 pm

KOCHA mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa anaamini uwekezaji mkubwa uliofanywa na Yanga kwa kusajili wachezaji bora ni miongoni mwa sababu kubwa za mafanikio ya kikosi hicho kilicho chini ya kocha Mrundi, Cedric Kaze.

Yanga imekuwa yamoto msimu huu ambapo mpaka sasa ndiyo mabingwa wa kombe la Mapinduzi na vinara wa Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya pointi 44 katika michezo 18 waliyocheza, huku wakiwa na rekodi ya kucheza michezo 22 ya mashindano rasmi bila kupoteza tangu kuanza kwa msimu. 

Mkwasa ambaye ameifundisha Yanga katika vipindi tofauti, ambapo msimu uliopita alihudumu kama kocha msaidizi ndani ya kikosi hicho amekuwa na wakati bora msimu huu akiiongoza Ruvu Shooting kukamatia nafasi ya tano kwenye msimamo na pointi zao 28 walizokusanya baada ya kucheza michezo 17.

Akizungumzia ubora wa Yanga msimu huu Mkwasa alisema: “Msimu huu Yanga imekuwa na  bajeti kubwa zaidi hivyo kumpa urahisi kocha kufanya usajili wa wachezaji bora na hata kuwa na kambi zenye mazingira mazuri zaidi, kwa upande wangu hili ni miongoni mwa sababu kubwa za wao kupata mafanikio makubwa waliyonayo”

CRYSTAL PALACE KUTHIBITISHA KUPATA SAINI YA JEAN MRUNDI WA YANGA AWAAHIDI MASHABIKI FURAHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply