Yanga SC

MTAMBO WA MABAO YANGA: UBINGWA BILA KUFUNGWA INAWEZEKANA

admin January 22, 2021 2:47 pm

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, Waziri Junior amesema kuwa anaamini kuwa upo uwezekano wa kikosi chao kuibuka na ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu bila kupoteza mchezo hata mmoja. 

Waziri aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea kwenye kikosi cha klabu ya Mbao aliyoichezea msimu uliyopita tayari ameifungia Yanga bao moja akilifunga kwenye mchezo wa raundi ya kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-1 walioupata dhidi ya KMC.

Licha ya kuwa na mwendo wa kusuasua ndani ya Yanga lakini nyota huyo akiwa na Mbao msimu iliyopita alimaliza akiwa kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa wafungaji bora baada ya kuweka kambani mabao 13.

Akizungumzia ubora wao msimu huu Waziri amesema: “Tumekuwa na msimu mzuri tangu kuanza kwa ligi na ndiyo maana mpaka sasa kikosi chetu kinaongoza msimamo wa ligi na hatujapoteza mchezo wowote.

“Ubingwa tulioupata kupitia michuano ya kombe la Mapinduzi umezidi kutupa ari ya kupambana zaidi na naamini tutafanya vizuri kwenye michezo ya mzunguko wa pili ambapo tunataka kutwaa ubingwa, na kama tutaendelea kupambana namna tunavyopambana basi inawezekana tukatwaa ubingwa bila kufungwa,”

ISHU YA BERNARD MORISSON KUWA NJE MIEZI SITA SIMBA IPO HIVI ISHU YA USAJILI MUDA WAKE UMEKWISHA, KAZI IHAMIE UWANJANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply