MARA baada ya mabosi wa Klabu ya Simba kumshusha kocha mpya kwa ajili ya kuwanoa makipa wanaoongozwa na kipa namba moja Aishi Manula, Beno Kakolanya na Salim Ally, kocha huyo ameanza rasmi mazoezi Januari 23.
Anaitwa Milton Nienov raia wa Brazil amekuja kuchukua mikoba ya Mwarami Mohamed ambaye alichimbishwa ndani ya Simba baada ya matokeo mabovu kwenye mechi mbili mfululizo ndani ya Ligi Kuu Bara.
Kocha huyo amewahi kufundisha katika Klabu za Polokwane City, Lamontville Golden Arrows FC, Super Eagles FC, Free State Stars FC za Afrika Kusini na Club de Regatas Vasco da Gama, Sport Club Recifie na Figueirense FC za Brazil.
Amesaini dili la miaka miwili kwa ajili ya kuhudumu ndani ya kikosi hicho chenye kazi ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara.
Leo pia kikosi cha Simba kimeanza mazoezi kujiandaa na Simba Super Cup ambayo itaanza siku ya Jumatano tarehe 27 Januari, 2021.
Mashindano hayo yanashirikisha timu tatu ambazo ni wenyeji wenyewe Simba, TP Mazembe na Al Hilal ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kujiaandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.