Simba SC

MNIGERIA WA SIMBA ATUA, MABEGI YAKE YAZUA MASWALI

admin January 23, 2021 2:47 pm


MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Simba raia wa Nigeria, Junior Lokosa amewasiri rasmi nchini Tanzania leo kwa ajili ya kukamilisha taratibu zake za kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Simba.

Kivutio kikubwa kwenye ujio wa Lokosa aliyepokelewa na Katibu Mkuu wa Simba, Dk. Arnold Kashembe ni wingi wa mabegi aliyokuja nayo ukizua maswali mengi kama amehamia moja kwa moja au vipi, kwani nyota huyo alikuwa na mabegi manne makubwa mawili na ya madogo mawili.

Lokosa ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo baada ya Mzimbabwe, Tatenda Perfect Chikwende na Mkongomani Gikanji Doxa na Taddeo Lwanga raia wa Uganda.

Lokosa mwenye umri wa miaka 27 ana uzoefu na soka la Afrika ambapo amewahi kucheza nchini Nigeria na Tunisia katika klabu za Esperance, Kano Pillars na First Bank.

NAMUNGO YATAMBIA USAJILI WAO MPYA YANGA PRINCESS HAIKAMATIKI, YAMALIZA MZUNGUKO WA KWANZA KILELENI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply