Home Simba SC GOMES : HUYU CHIKWENDE NI BALAA…, LUKOSA APEWE MUDA..!!

GOMES : HUYU CHIKWENDE NI BALAA…, LUKOSA APEWE MUDA..!!


KOCHA mpya wa Simba, Didier Gomes ameukubali uwezo wa nyota mpya, Mzimbabwe Perfect Chikwende lakini akasema Mnigeria Junior Lokosa anahitaji muda.

Kocha mpya wa Simba, Gomes tangu ameanza kazi nchini amesimamia mazoezi ya timu hiyo katika awamu tatu na kutoa mtazamo wake juu ya nyota hao wawili wapya na wachezaji wengine pia.

Gomes alisema kwa jinsi wamefanya mazoezi amebaini kwa upande wa nyota wa kigeni, Chikwende amemfurahisha kwa kufanya vizuri zaidi mara kwa mara katika maeneo mengi.

“Awali nilikuwa namsikia na nilipata muda wa kumfuatilia kwa kuangalia mechi zake za nyuma, lakini baada ya kuwa naye, nimebaini ni moja ya wachezaji bora ambao tumesawajili.”

“Chikwende amekuwa akifanya vizuri katika kila zoezi ambalo tunafanya na ameonyesha ni mchezaji anayependa ushindani na kutamani kucheza zaidi,” alisema Gomes.

Aliongeza “Muda mfupi ambao nimekaa naye nimebaini anaweza kuwa na mpira mguuni na ngumu kupoteza, anapiga pasi nzuri pamoja na kupenda kupiga chenga walinzi wa timu pinzani, akiwa na mpira ana uwezo wa kukimbia pamoja na mengine mengi ambayo nitayabaini kutoka kwake katika siku zijazo.

“Kijumla nikiendelea kuwa naye katika timu na vile nilivyomwona Chikwende nina imani anaweza kufanya zaidi ya hivyo,” alisema Gomes.

“Lokosa anahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi mbalimbali ili kuwa fiti kimwili kwanza ili kuweza kushindana na wachezaji wa timu pinzani, lakini kuzoea kucheza mpira ili kutimiza majukumu yake ya kufunga,” alisema.

MSIKIE TRY AGAIN

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ alifichua wanahitaji kuwa na mawinga wenye maudambwi udambwi kama wa Luis Jose ndio maana wakamsainisha Chikwende.

“Tunahitaji kuwa na mawinga wenye nguvu na mbio kama anvyofanya na Luis na kwa Chikwende ni hatari, subirini ligi ianze mtajua nini tunakimaanisha kuhusu usajili huo.”

“Chikwende ni kama Morisson tu na Simba ya sasa inasajili wachezaji kama hawa ambao watakuwa na tija na umuhimu ndani ya timu na sio ilimradi kusajili tu, tunamleta mtu ambaye anakuwa na faida ndani ya timu, wao wanaongoza ligi lakini nafasi hiyo ni ya kwetu sisi Simba hatuna mzaha kabisa, ubingwa wa Ligi lazima tuutetee na hata FA, huko Ligi ya Mabingwa ndio tunapambana tufike hatua ya juu zaidi,” aliongeza.

SOMA NA HII  BAADA YA KUILIZA YANGA KWA FEI TOTO....SASA ZAMU YA SIMBA...MABOSI AZAM WAAPA KUMBEBA STAA HUYU..