Home Yanga SC SARPONG APEWA ‘LAST CHANCE’ YANGA

SARPONG APEWA ‘LAST CHANCE’ YANGA

 


INAELEZWA kuwa bado kocha wa Yanga, Cedrick Kaze anamatumaini na mshambuliaji wake, Michael Sarpong hivyo ameona anastahili nafasi nyingine tena ya kuonyesha makali yake ndio maana hakukatwa wakati wa dirisha dogo.

Taarifa za chini chini zinasema kama mshambuliaji huyo atashindwa kuonyesha makali yake kwenye duru la pili basi Kaze hatakuwa na chamswalia mtume.

Licha ya kwamba matumaini makubwa ya Kaze yapo kwa Fiston Abdulrazak raia wa Burundi lakini anaamini kuwa Sarpong anaweza kubadili mambo na kuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi chake kinachoongoza msimamo wa ligi.

SOMA NA HII  KAZE : HII YANGA KAMA SIO AUCHO NA FEI TOTO HALI INGEKUWA SIO...