Home Simba SC KUMBE SVEN ALIBWAGA MANYANGA KIMYAKIMYA, SIMBA HAWAKUTAKA KUACHANA NAYE

KUMBE SVEN ALIBWAGA MANYANGA KIMYAKIMYA, SIMBA HAWAKUTAKA KUACHANA NAYE


UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa haukuwa na mpango wa kuachana na Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba na alibwaga manyanga Januari 7.

Sven alisepa ndani ya Simba mazima ikiwa ni siku moja baada ya Januari 6 kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum umewapa tiketi Simba kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Simba, Crestius Magori amesema kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba,(Barbara Gonzalez) alipigiwa simu na watu kutoka sehemu aliyokuwa anakaa Sven na kuambiwa kuwa amebeba kila kitu mpaka viatu.

“Hatukuwa na mpango wa kuachana na Sven ila yeye mwenyewe aliamua kuondoka na CEO,(Barbara) alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mbona kocha amebeba kila kitu kutoka kwa watu wa sehemu aliyokuwa anakaa.

“Ilikuwa ni asubuhi wakati huo timu ilikuwa inajiaandaa kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi.

“CEO alimpigia simu Sven ambapo alisema kuwa bado yupo hana mpango wa kuondoka ila timu imeanza safari mchana ndipo anamwambia CEO kwamba kuna matatizo ya kifamilia anahitaji kuondoka.

“Hata ambapo aliambiwa kwamba kama ishu ni familia basi ilete hapa Tanzania kuna shule akasema kwamba ana ofa kibao ikiwa ni pamoja na Morocco ambapo ni karibu na Ublelgiji, sasa hapo hatukuwa na namna ikabidi tumuache aondoke,” .

Sven kwa sasa yupo ndani ya Klabu ya FAR Rabat ya Morroco akiwa ni kocha mkuu na Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa.


SOMA NA HII  KISA UCHAGUZI ...KADUGUDA ALIAMSHA SIMBA SC...AANIKA SAFARI YA BARBARA QATAR..