Home Taifa Stars STARS BADO INA MATUMAINI CHAN, WAWILI HATIHATI KUIKOSA NAMIBIA

STARS BADO INA MATUMAINI CHAN, WAWILI HATIHATI KUIKOSA NAMIBIA

LICHA ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Zambia kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 19 nchini Cameroon ukiwa ni wa kufuzu Chan bado Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije anaamini kwamba nafasi bado ipo kwa Stars.

Ikiwa ipo kundi D, Uwanja wa Limbe iliyeyusha mazima pointi tatu kwa kufungwa mabao mawili mchezo wa ufunguzi na imebakiwa na mechi mbili za kusaka ushindi.

Kesho Jumamosi pia inashuka uwanjani kusaka ushindi mbele ya timu ya Taifa ya Namibia na kete yake ya mwisho ni Januari 27 dhidi ya Guinea ambapo ili iweze kufuzu kutinga hatua ya robo fainali.

Kwa sasa ni wachezaji wawili ambao wanahitaji ripoti kutoka kwa dakatri ili kujua kama wanaweza kucheza ambao ni mshambuliaji John Bocco na beki wa kati Ibrahim Ame ambao ni majeruhi.

 Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Stars amesema kuwa vijana wapo tayari kwa mapambano na wana imani ya kupata matokeo.

“Mchezo wa kwanza tulianza vizuri ila makosa ambayo tuliyafanya yalitugharimu, tutayafanyia kazi ili mechi zetu zilizobaki tufanye vizuri, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kikubwa sapoti,” .

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA NIGER LEO....KOCHA TAIFA STARS AANIKA JAMBO LAKE WAZI...