Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA NIGER LEO….KOCHA TAIFA STARS AANIKA JAMBO LAKE WAZI…

KUELEKEA MECHI NA NIGER LEO….KOCHA TAIFA STARS AANIKA JAMBO LAKE WAZI…

Taifa Stars

LEO Novemba 18 2023 timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa jijini Marrakech, Morocco ambapo wachezaji wa Stars Novemba 17 walifanya mazoezi katika mji huo Uwanja wa Marrakech Annex One.

Adel Amrouche Kocha Mkuu wa Stars amesema wapo tayari kwa mchezo huo.

“Tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumefika salama na maandalizi yapo vizuri. Kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuwa kwenye hali nzuri ya utafuta matokeo.

“Mpira unahitaji furaha na furaha inapatikana kwenye matokeo mazuri hivyo tutapambana kufanya vizuri ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wetu muhimu,”.

SOMA NA HII  HUU MPANGO WA SIMBA WAWATISHA MABEKI WYDAD