Home Habari za michezo HUU MPANGO WA SIMBA WAWATISHA MABEKI WYDAD

HUU MPANGO WA SIMBA WAWATISHA MABEKI WYDAD

Wakati klabu ya Simba ikiendelea na maandalizi kabla ya kuivaa Wydad Casablanca kesho jijini Marrakech, Morocco huku beki wa timu ya Wydad, Arsene Zolla akionekana kuingiwa ubaridi kwa kuihofia Simba.

“Unakumbuka tulivyocheza nao huku mara ya mwisho walionyesha mchezo mkubwa lazima unapokwenda kukutana na timu kama hiyo mnatakiwa kuwa makini,” alisema Zolla.

“Wana wachezaji waliokomaa sana na mashindano kama haya na unaona sasa wamemuongeza ndugu yangu Fabrice (Ngoma) ni mchezaji mkubwa tunamjua na anaijua Wydad utaona kwamba timu yao sio mbaya.” Aidha Zolla aliongeza hatua ya kikosi cha Wydad kushinda mabao 3-1 mechi ya Ligi Kuu mbele ya Mouloudia Oujda, ni hatua nzuri ya kujiandaa na mchezo huo wa kesho wakiwa na morali.“Tulikuwa hatujashinda mechi nne mfululizo, lakini sasa angalau tumepata nguvu kuikabili Simba.”

SOMA NA HII  WAJUE WALIOPIGWA 'PANGA' SIMBA, MANARA ANAWAKERA ,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI