Home Simba SC WINGA MKONGO AFUNGUKIA DILI LAKE SIMBA

WINGA MKONGO AFUNGUKIA DILI LAKE SIMBA


BAADA ya kiungo Mkongo Karim Kinvuid Kiekie kuhusishwa kumalizana na klabu ya Simba, hatimaye kiungo huyo amefunguka kuwa hajafanya mazungumzo na uongozi wa Simba

Kiekie alicheza katika mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Congo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar na kumalizika kwa sare ya bao 1-1,kwa sasa kiungo huyo yupo katika kiosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya CHAN inayoendelea kufanyika nchini Cameroon.

Akizungumzia kuhusu dili hilo Kiekie amesema: “Sijafanya mazungumzo na Simba juu wao kuhitaji huduma yangu, yote ambayo unayasikia wewe na mimi ninayasikia hivyohivyo ndio maana nayaacha yabaki kuwa tetesi ila kama itatokea wananihitaji basi kila kitu kitafahamika,”

Kiekie mwenye umri wa miaka 19 kwa sasa anakipiga katika klabu ya DC Motema Pembe ya nchini Kongo ambapo  nchini humo anachukuliwa kama mmoja kati ya wachezaji bora wanaochipukia kwa kasi.

SOMA NA HII  KUHUSU HALI YA INONGA DAKTARI AFUNGUKA HAYA