Home Simba SC ZAHERA: SIMBA HAWANA HELA YA KUMCHUKUA IBENGE

ZAHERA: SIMBA HAWANA HELA YA KUMCHUKUA IBENGE


 MWINYI Zahera aliyekuwa kocha ndani ya Klabu ya Yanga kabla ya kuchimbishwa msimu wa 2019/20 amesema kuwa Simba hawana mkwanja wa kumchukua Florent Ibenge awe mbeba mikoba ya Sven Vandenbroeck.


Imekuwa ikielezwa kuwa Ibenge amepewa dili na mabosi wa Simba akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo pia anafundisha timu ya Taifa ya Congo.


Ibenge amesema kuwa kweli aliwahi kuzungumza na Simba kuhusu kuhitaji huduma yake ila mazungumzo yao hayakufika sehemu nzuri.

Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina FC amesema haitakuwa rahisi kwa Ibenge kuibuka ndani ya Simba.

“Simba hawana pesa ya kumchukua Kocha Florent Ibenge kuwa kocha wao mkuu,wanaosema hivyo waongo.

“Ibenge ni kocha mzuri ila hawezi kuja kwa Simba, najua hawana hela ya kumchukua kocha huyo kwa sasa,” .
SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI KUHUSU BEKI OUATTARA NA ANAYOYAPITIA SIMBA...TAARIFA RASMI YATOLEWA...